Lyrics Of The Song Unapojaribiwa
Song ID 3488
unapojaribwa usitende dhambi unapojaribiwa jua Mungu yupo unapojaribiwa usivunjike moyo hilo jaribu lako Mungu ameliona jaribu ni mlango wa kuinuliwa jaribu ni daraja la mafanikio jaribu ni darasa la watakatifu nimejifunza hilo kwa kuwa Mungu amefanya wakati wa jaribu watu wanakucheka wakati wa jarabu unadharauliwa wakati wa jaribu unajiona mpweke hilo jaribu lako Mungu ameliona unapojaribiwa usilipe kisasi unapojaribiwa usimchukie huyo unapojaribiwa usitazame adui yako wewe mtazame Mungu umwombe rehema wakati wa jaribu ikiwezekana huyo anayetumiwa muombee rehema wakati wa jaribu Mungu akikupa neema pema na matatizo lia pamoja naye unapojaribwa usitende dhambi unapojaribiwa jua Mungu yupo unapojaribiwa usivunjike moyo hilo jaribu lako Mungu ameliona inawezekana uko kwenye mateso inawezekana umekata tamaa inawezekana umedharauliwa hilo jaribu lako Mungu ameliona inawezekana ni wakati wa mateso inawezekana marafiki wamekimbia inawezekana ndugu amekutenga hilo jaribu lako Mungu atalijibu inawezekana uko wakati mbaya inawezekana kipindi cha kuonewa inawezekana marafiki wamekutenga hilo jaribu lako Mungu ameliona muombe Mungu jibu lako liko muombe Mungu leo atatenda muombe Mungu leo atakujibu hilo tatizo lako Mungu analijua usikate tamaa mwamini Yesu usikate tamaa mwambie Yesu rudia x10
Unapojaribiwa.video.mp4 YouTube
Hits: 6