Ibada Lyrics ibada_lyrics Maneno Saba Ya Msalabani

Maneno Saba Ya Msalabani

Lyrics Of The Song Maneno Saba Ya Msalabani

Song ID 2609

maneno saba ya msalabani inafaa sana tuyafuate mwokozi aliyanena mwenyewe alipokuwa msalabani na tumwimbie mwana kondoo msalabani na tumwimbie kwani aishi milele walipofika pafuvu la kichwa wakamsulubu na wahalifu neno lake la kwanza ndilo Bwana wasamehe hawajui watendalo mwana alipomwona mama yake akamkabidhi kwa wanafunzi mama tazama huyo mwana wako nawe tazama mama yako huyo mhalifu huyo alimwomba amkumbuke kwenye ufalme amini leo hivi utakuwa na mimi mjini huko peponi ilipotimia saa ya sita alipaza sauti akalia eli eli lama sabakitani Mungu wangu mbona umeniacha hapo msalabani alikaa kwa ukombozi wa dunia hii akasema kuwa naona kiu ili andiko lipate timia alichukua mzigo mzito hukumu ya dunia ya maasi akatimiza yaloyomleta akasema kuwa imekwisha giza la saa sita hadi tisa kweli kiamba kilipasu uka akalia ee baba mikononi mwako naiweka roho yangu

Maneno Saba Ya Msalabani.mp3

Maneno Saba Ya Msalabani.video.mp4 YouTube

 

Hits: 2

Leave a Reply

Related Post