Ibada Lyrics ibada_lyrics Mimi ni Mama

Mimi ni Mama

Lyrics Of The Song Mimi ni Mama

Song ID 3156

oiyee oiyee nalia nalia mimi mzazi mimi ni mama mimi ni mama mimi ni mama nalilia watoto wangu mimi ni mama mimi ni mama mimi ni mama najutia kosa langu mimi ni mama kwa wote wenye mwili mimi ni mama kwa wakubwa kwa wadogo mimi ni eva mimi ni awa naomboleza najutia kosa langu baba yangu Mungu niangalie leo nimekuja kwako kwa huzuni nyingi ni kweli baba uliniamini mimi ukanipa dunia niwe mama wa wote nilikosea sana nilipokula tunda ulionikataza ninajuta leo matokeo ya dhambi niliyoifanya inatesa watoto wangu niliyowazaa mimi ni mama mimi ni mama mimi ni mama nalilia watoto wangu mimi ni mama mimi ni mama mimi ni mama najutia kosa langu waliotoka tumboni mwangu tazama sasa baba hawaelewani caini huyu anamuua abeli watoto wangu wanamalizana mbio za shilingi zamaliza watoto wangu wengine kwa risasi wengine kwa mabomu wengine wako magerezani baba Mungu okoa watoto wetu wengine wafaa mahosipitalini hawana shilingi ya kununua kidonge tazama wengine wako uchochoroni hawaendi shule wanacheza gemu mimi ni mama mimi ni mama mimi ni mama nalilia watoto wangu mimi ni mama mimi ni mama mimi ni mama najutia kosa langu uchungu waniuma nikiwaona watoto wanavyoteseka katika dunia hii nalilia binti zangu waja wazito wamejaa makovu katika tumbo yao mara pressure mara kifafa wapoteza maisha katika uzazi neno lako lasema tutazaa kwa uchungu operesheni hizi zinatoka wapi kina mama wote njoni tuomboleze tuwalilie watoto wetu wasiangamie tuombee ndoa tuombe amani ya nchi yetu isije toweka neno linasema waiteni wanawake waliostadi kwa kuomboleza wawefundisha mabinti zao kuomboleza machozi yao yabubujike kwa maana mauti imepandia dirishani ipate kukatilia mbali watoto wetu Bwana wangu Yesu wewe ulisema enye kina mama msinililie mimi bali jililieni nafsi zenu na watoto wenyu mimi ni baba mimi ni baba mimi ni baba najutia watoto wangu mimi ni baba mimi ni baba mimi ni baba naombea watoto wangu naombea nchi yangu tanzania naombea kizazi chetu ooh Yesu africa ombea dunia yote

Mimi ni Mama.mp3

Mimi ni Mama.video.mp4 YouTube

 

Hits: 11

Leave a Reply

Related Post