Ibada Lyrics ibada_lyrics Nimewasamehe Wote

Nimewasamehe Wote

Lyrics Of The Song Nimewasamehe Wote

Song ID 2185

mmmh ooh oooh nilipokuwa mtoto nilizaliwa kama wewe viungo vyote vya mwili vilikuwa kama wewe ghafla dunia mambo yakageuka nikajikuta kiugo kimoja kimeniondokea mimi nikajua kuwa mwisho wa mambo yote imefika wala sifai nikaona dunia imenitupa nikaona dunia imenidharau nikajidharau mwenyewe nikajua sasa mimi sifai tena niliwanungunikia wote waliohusika kwa haya mambo roho ya kisasi ikaja juu yangu nikajua sasa na mimi nitalipa kisasi kumbe kunaye Mungu Mungu wa visasi akaniambia solomon nina mpango na wewe lazima piga hatua uwasamehe kwanza ooh nikabishana na Mungu wote walionitendea mabaya mimi siwezi wasamehe moyoni mwangu Bwana kaniambia wataka nitumike na wewe nina ahadi zuri na wewe kuhusu dunia hii ukitaka nitumike na wewe uwaachilie wote uliowaweka moyoni mwako nikapiga hatua nikawasamehe wote walionikosea Bwana akatumika na mimi ooh refrain nimewasamehe wote nimewasamehe wpte nimewasamehe kutoka moyoni mwangu nimewasamehe wote nimewachilia kutoka moyoni mwangu tumekunywa damu damu ya Yesu tumekula na mwili wa Yesu ooh mwili wa Yesu ni msamaha aah tujikane wenyewe mara nyingi tumeonekana wajinga duniani dunia imeshindwa kutuelewa wakristo eeh umetendewa mabaya lakini neno linasema kubali nenda ukaombe msamaha ki kawaida ya dunia ukinitendea mabaya lazima ooh ieleweke lakini kwetu sisi wakristo ukinitendea mabaya mimi lazima nikusamehe sababu nisipokusamehe baba yetu wa mbinguni na yeye hawezi nisamehe haijalishi unapitia nini kama wewe umeokoka huwasamehe waliokukosea ooh eeh husifanye moyo walo jela kuwafungia wat amua leo uwaondoe ili Mungu wetu akubariki samehe jirani yako Mungu na yeye atakusamehe nimewasamehe wote nimewasamehe wpte nimewasamehe kutoka moyoni mwangu nimewasamehe wote nimewachilia kutoka moyoni mwangu ni vigumu jamani mara nyingi kuna mambo ambayo tunapitia mwenzako mwanadamu anakupitisha kwa mambo mazito lakini unapaswa ufanyeje ashurukuriwe Mungu sababu neno la Mungu linasema tusamehe tu na tumevaa mwili wa Yesu tumekunywa damu ya Yesu kumbuka msalabani Yesu aliwaponya watu viwete wakatembea mabubu wakaongea akawalisha watu zaidi ya elfu tano lakini wale watu ndio walimuweka msalabani mwisho msalabani ikasema baba wasamehe huwasamehe kumbuka stephano stephano alikuwa anapigwa mawe alipokuwa anapigwa mawe bibilia inasema stephano kaambia baba huwasamehe maana hawajui wanalolitenda bibilia inasema stephano akaona mbingu zinafunguka kwenye msamaha kuna nguvu kwenye msamaha kuna uwezo stephano hakujali tena mawe wanayomtupia wanayomchapa lakini stephano alikuwa ameona mbingu zimefunguka na tayari anakwenda kupokelewa msamahe jirani yako kusudi uone mkona wa Mungu usimfungie kwenye moyo wako utakuwa umujizuilia baraka yako msamehe muachilie tu maana tumevaa mwili wa Yesu na tumekunywa damu ya Yesu ooh Yesu tusaidie kuwasamehe waliotukosea

Nimewasamehe Wote.mp3

Nimewasamehe Wote.video.mp4 YouTube

 

Hits: 7

Leave a Reply

Related Post