Ibada Lyrics ibada_lyrics Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku hiyo Aliponijia

Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku hiyo Aliponijia

Lyrics Of The Song Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku hiyo Aliponijia

Song ID 915

tangu siku hiyo aliponijia akae moyoni mwangu sina giza tena ila mwanga pia kwa Yesu mwokozi wangu amani moyoni mwangu kwa Yesu mwokozi wangu sina shaka kamwe kwa sababu yeye yu nami moyoni mwangu sina haja tena ya kutanga tanga ndiye kiongozi changu dhambi zangu zote zimeondolewa na Yesu mwanawe Mungu amani moyoni mwangu kwa Yesu mwokozi wangu sina shaka kamwe kwa sababu yeye yu nami moyoni mwangu matumaini yangu ni ya hakika katika mwokozi wangu hofu zangu na hamu zimeondoka kwa kuwa ninaye Yesu amani moyoni mwangu kwa Yesu mwokozi wangu sina shaka kamwe kwa sababu yeye yu nami moyoni mwangu siogopi tena nikiitwa kufa yu nami daima Yesu mlango wa mbingu ni Yesu mwokozi tapita humo kwa damu nitaketi na Yesu huko milele nimsifu mwokozi wangu nina raha moyoni majira yote kwa Yesu mwanawe Mungu

Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku hiyo Aliponijia.mp3

Amani Moyoni Mwangu Tangu Siku hiyo Aliponijia.video.mp4 YouTube

 

Hits: 10

Leave a Reply

Related Post