Ibada Lyrics ibada_lyrics Soma Mwanangu

Soma Mwanangu

Lyrics Of The Song Soma Mwanangu

Song ID 2016

mshike sana elimu usimwache aende zake ni maneno ya Mungu kutoka kwenye vitabu vitakatifu mimi enzi zangu maneno hayo si kuyajua nilifanya mchezo sikuweka uzito kwenye elimu hivyo nilishindwa kusoma ndio maana namuomba Mungu mtoto wangu usome hivyo mimi baba yako nilishindwa kusoma ndio maana namuomba Mungu mtoto wangu usome soma baba yako anapenda mwanangu usome mama yako anapenda mwanangu usome namuomba Mungu akusaidie sana mwanangu usome namuomba Mungu akupiganie wewe mwanangu usome usifanye mchezo ukiwa darasani mwanangu mimi na mama yako tunapenda sana usome ukifanya mchezo maisha yetu mwenyewe unayajua ukifanya mchezo tutakuwa wageni wa nani soma soma mwanangu soma we soma mwanangu pengine utakuja kutuokoa we baadaye mimi baba yako sikubahatika kusoma soma mwana usome wewe pengine unaweza okoa familia yetu kazi ya ulinzi ni ngumu nakulilia we usoma soma we mwanangu mama yako pia anapenda usome nabeba kirungu nangatwa na mbu usiku kucha kwa ajili yako mwanangu soma we mama yako anapenda mwanangu soma maisha bila elimu ni magumu soma we mimi na mama yako hatuchoki kukuombea Mungu akusaidie nimebeba zege pesa yote nimepeleka shule soma robo tatu ya mshahara wangu wote nimepeleka shule mama yako anapenda mwanangu soma tumeuza ngombe pesa zote tumepeleka shule mama yako anapenda mwanangu usome tunamwomba Mungu wa mbinguni afanye njia mama yako kauza chapati pesa yote tumepeleka shule mama yako anapenda mwanangu soma mambo niliyoyafanya nikiwa shule sitaki hata kuyakumbuka moyo wangu unauma kila nikikumbuka maisha magumu ninayoishi uzembe wangu umechangia nilifanya mchezo nikiwa shule mwana niliona sifa daftari yangu kujisahishia leo hii najuta natamani kusoma niliona sifa kutoroka shule kupitia dirishani leo hii najuta natamani kusoma napendwa na wasupu lakini lugha inanikosa leo hii najuta natamani kusoma nikimwona mzungu kwa mbali nabadilisha njia naogopa asije akanisemesha how are you na lugha sijui soma mwanangu soma wee mama yako anapenda mwanangu soma baba yako anapenda mwanangu usome mama yako anapenda mwanangu usome bony mwaitage feat bahati bukuku

Soma Mwanangu.mp3

Soma Mwanangu.video.mp4 YouTube

 

Hits: 4

Leave a Reply

Related Post