Ibada Lyrics ibada_lyrics Mtegemee Yesu

Mtegemee Yesu

Lyrics Of The Song Mtegemee Yesu

Song ID 1360

mambo mengi yakupata ndugu yanayokuumiza moyo hata ukimwomba Mungu waona kama vile amekutenga maisha magumu shida tupu wapepeshwa dunia nzima unapapasa hapa na pale bila kupata msaada umeanza kukata tamaa imani yako inayumbayumba unajisikia upweke umeachwa kama yatima utokako ni mbali sana kiasi kwamba huwezi rudi mbele huenda kunako giza umekosa matumaini magumu shida yakupatayo ndugu ni ya muda kidogo kamwe yasikutenganishe na yule rafiki wa kweli hebu itegemee ahadi yake kwamba atakuwa nawe hata kwenye wakati huo mgumu mtegemee Yesu umesongwa nazo shida nyingi lakini mkumbuke ayubu alivyozidiwa nayo majaribu akasimama imara japo yako imefanywa wimbo nao waumini wenzako sawa na wale marafiki za ayubu walivyomcheka usiiruhusu shida yako kukunyakua mkononi mwa Bwana jibu lako ni yeye pekee tegemeo na kimbilio hata wenzako wakutenge vumilia utayashinda ndugu jipe moyo mtetezi yupo magumu atarahisisha magumu shida yakupatayo ndugu ni ya muda kidogo kamwe yasikutenganishe na yule rafiki wa kweli hebu itegemee ahadi yake kwamba atakuwa nawe hata kwenye wakati huo mgumu mtegemee Yesu umeanza kukata tamaa imani yako inayumbayumba unajisikia upweke umeachwa kama yatima utokako ni mbali sana kiasi kwamba huwezi rudi mbele huenda kunako giza umekosa matumaini usiiruhusu shida yako kukunyakua mkononi mwa Bwana jibu lako ni yeye pekee tegemeo na kimbilio hata wenzako wakutenge vumilia utayashinda ndugu jipe moyo mtetezi yupo magumu atarahisisha

Mtegemee Yesu.mp3

Mtegemee Yesu.video.mp4 YouTube

 

Hits: 2

Leave a Reply

Related Post