APEWE SIFA | Mtakatifu Kizito Makuburi Choir
Sifa na utukufu vyote ni kwa Mungu hee heee
Sifa na utukufu vyote ni kwa Mungu hee hee} X2
Utukufu nakupa wewe,
utukufu nakupa we,
Sifa na heshima nakupa we,
Ewe mwenyezi unaweza X2
Nguzo ya moto aliwasha, nilindwe usiku,
Nayo ya wingu akashusha nipite mchana
Na-kumbuka mapito yote, niliyopitia,
Nakumbuka na njia zote, nilizopitia
Tazama Mungu tazama wewe,
Tazama Mungu tazama wewe
Tazama Mungu tazama wewe
unatimiza ahadi yako
Tazama Mungu tazama wewe
(tazama Mungu ) ni mwaminifu
Tazama Mungu tazama wewe
unatimiza ahadi yako
Utukufu nakupa wewe,
utukufu nakupa we,
Sifa na heshima nakupa we,
Ewe mwenyezi unaweza X2
Jemedari mwenye maguvu, yule Goliathi,
Akamlaza kwa kombeho, mkononi mwangu
Nakumbuka alikemea, mawimbi ya maji,
Na-kumbuka yalimtii, nikafika ng’ambo
Tazama Mungu tazama wewe,
Tazama Mungu tazama wewe
Tazama Mungu tazama wewe
unatimiza ahadi yako
Tazama Mungu tazama wewe
(tazama Mungu ) ni mwaminifu
Tazama Mungu tazama wewe
unatimiza ahadi yako
Utukufu nakupa wewe,
utukufu nakupa we,
Sifa na heshima nakupa we,
Ewe mwenyezi unaweza X2
a) Bahari haiwezi kutuzuia –
Tunatembea bila mitumbwi
Na maji yanageuka kuwa ukuta –
Mungu mwenyewe ni mtumbwi wetu tunavu-ka
b) Maana amesema tumfuate –
Tunatembea bila mitumbwi
Mizigo itulemeayo tukampe –
Mungu mwenyewe ni mtumbwi wetu tunavu-ka
c) Muhimu tumwendee tukiamini –
Tunatembea bila mitumbwi
Na hata juu ya maji tutakanyagaa
Mungu mwenyewe ni mtumbwi wetu tunavu-ka
{ Alimkumbuka Daudi mtumishi wake Aka-mkweza
Akawavusha waisraeli katika maji bila mitumbwi } X2
Apewe, apewe, apewe sifa kuu Mungu
Ape-we, apewe, milele milele
Apewe apewe, ape-we sifa kuu Mungu
apewe, apewe Sifa na utu-
kufu vyote ni kwa Mungu hee hee
mtumbwi in English like canoe, rowboat and many others.
Hits: 23