Ibada Lyrics ibada_lyrics Napokea kwako

Napokea kwako

Lyrics Of The Song Napokea kwako

Song ID 1575

maisha magumu sana nimepitia nikajaribu kutafuta msaada sikupata nikaendea mwanadamu mwisho akanidharau kumbe msaada wa mwanadamu unatoka kwa Mungu nilijua yapo wenye haki ya kubarikiwa kumbe baraka ni haki ya kila mmoja nimebadili wazo langu namwelekea Mungu kwake msaada wangu unapatikana msaada wa mwanadamu ni wa muda mfupi na ni zamu yangu kubarikiwa we wakati ni huu wa kubarikiwa zamu ni yangu sasa kupokea nimechoshwa na shida za dunia napokea kwako baba napokea kwako napokea kwako baba napokea kwako napokea kwako Yesu napokea kwako napokea kwako baba napokea kwako nimeamua kwenda zaidi na zaidi nimejipanga hadi nione matunda yake yale Mungu amewekeza ndani yangu najua Mungu yupo kazini kunikamilisha akisema nimebarikiwa nimebarikiwa tu hata ukipinga leo mimi nimebarikiwa tu mlima gani kuu sana usiloungoa jaribu gani kuu sana usiloliweza chozi gani zito kwako usilolifuta ombi gani kubwa sana usilolijibu wakati ni huu wa kubarikiwa zamu ni yangu sasa kupokea nimechoshwa na shida za dunia napokea kwako baba napokea kwako napokea kwako baba napokea kwako napokea kwako Yesu napokea kwako napokea kwako baba napokea kwako

Napokea kwako.mp3

Napokea kwako.video.mp4 YouTube

 

Hits: 3

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Post